Pichani ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ,Atupele Mwakibete ama Mamlaka ya Bandari mkoani Tanga kufanya kila jitihada kukamilisha mchakato unaohusu kuliwezesha Shirika la Reli TRCili kuwezesha kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya reli ndani ya eneo la Bandari ya Tanga.
NA SOPHIA WAKATI, TANGA.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ,Atupele Mwakibete ameitaka Mamlaka ya Bandari kufanya kila jitihada kukamilisha mchakato unaohusu kuliwezesha Shirika la Reli TRC kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya reli ndani ya eneo la Bandari ya Tanga.
Amesema lengo la kukamilika kwa hatua hiyo ni kurejesha miundombinu ya reli iliyokuwa imeondolewa wakati wa utekelezaji mradi wa maboresho Bandari ya Tanga unaotarajiwa kukamilika na kukabidhiwa rasmi hapo April 4 mwaka 2023.
Amesema Urejeshwaji wa reli hiyo utasaidia kuleta tija zaidi kutokana na mizigo itakayokuwa ikiteremshwa na Meli Bandarini kuweza kusafirishwa kirahisi kwa njia ya reli kwenda maeneo mengine baada ya kutoka Bandarini.
Naibu Waziri huyo wa uchukuzAtupele aliyasema hayo mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi Bandari ya Tanga ambapo alipata fursa ya kuzungumza na Wafanyakazi wa Bandari hiyo.
Mambo mengine ambayo Naibu Waziri ameagiza yafanyiwe kazi kwa haraka ukiacha urejeshwaji wa reli ni juu ya suala la eneo la utanuzi Bandari ya Tanga na mambo ya ardhi yaliopo kwa Kamishna husika.
Huku Jambo jingine ni ufuatiliaji eneo la Usagara pia linalohusu ardhi, na mchakato wa Bandari kavu ambayo inatarajiwa kuwekwa huko Mwambani.
Kutokana na hayo, Naibu Waziri ameagiza uongozi Bandari ya Tanga kulifanyia kazi kwa haraka suala la Bandari kavu kwa maelezo kuwa katika mwaka ujao wa bajeti kuna fedha zilizotengwa kwa umuhimu wa suala hilo.
"Lazima tuwe na miundombinu nyingine wezeshi kupata meli kubwa zaidi.juzi tumepokea meli yenye urefu Mita 190, eneo hili lina urefu Mita 450 manake zikiwa Meli mbili tayari eneo halitoshelezi"alisema Naibu Waziri akisisitiza maagizo ya Viongozi kutekelezwa.
Aliongeza;"wenzetu Duniani wana Meli kubwa zaidi urefu zaidi ya Mita 450 hivyo ikija Meli moja itaanza mwanzo wa ghati hadi mwisho nyingine zitasubiri, hivyo kwa hayamtaendelea kushauriana zaidi kuyasimamia"alisema Naibu waziri huyo Atupele.
Kwa upande wake Mhandisi kutoka bandari makao makuui,Hamisi Ngutu alisema, mradi wa ujenzi kuongeza ghati Bandari ya Tanga ni wa kimkakati ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 98%.
Kaimu meneja wa bandari,Peter Milanzi awali alisema uongozi wa Bandari ya Tanga imetoa wito kwa wadau na watumiaji wa kuitumia bandari hiyo iliyokuwa tayari kwa kuwapatia huduma zenye ubora.
Alisema licha ya wito huo, lakini pia uongozi huo umesema umejiandaa vyema kukabiliana na ushindani wa soko huku ukiahidi kuwahudumia vizuri wateja wake.
"Wadau wote tuendelee kushirikiana vyema Bandari yetu inaendelea kutumika na watu mbalimbali, tuko tayari kuchapa kazi ili kuleta faida kubwa target kwa mwaka ni kuhudumia tani mil tatu kutoka tani 750,000.
Mwakilishi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Amon Kiyomo alimhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa maelekezo aliyoyatoa yatasimamiwa huku akisema kwa vile fedha za ujenzi wa reli zimeshapatikana kazi husika itafanyika haraka.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment