Friday, 21 April 2023

KAMANDA MWAIBAMBE,AWATANGAZIA KIAMA WALIOJIPANGA KUFANYA UHALIFU SHEREHE ZA S/KUU YA Eid MUBARAKA,,,HASA WANAOTUMIA PIKIPIKI ZISIZO NA NAMBA KUPORA WANANCHI,,,

Picha katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Jijini Tanga kuelekea s/kuu ya Eid Mubaraka imeeleza jinsi ilivyojipanga kudhibiti vitendo vya uhalifu ambapo amesema wataimarisha usalama na kuhusu kumbi za Disco amesisitiza wamiliki kufuata sheria zilizopo,akiwa na maadhi ya maafisa wa jeshi la polisi mkoani hapo.

Pia amewataka wananchi kuacha tabia ya kuchukua sheria mkononi kumpiga mtu au kupigia kelele ya mwizui ili kunusuru mauaji kwa watu wasio na hatia kwa jamii mkoani hapa.

Kamanda Mwaibambe pia amesema wamefanikiwa kukomesha mtandao wa uhalifu maeneo mbalimbali ikiwemo wale ambao ni sugu,sasa hivi kazi yetu ni kuvuna kwa kuwanasa kwa kutumia Zone iliyopo.

NA SOPHIA WAKATI, TANGA
OPERESHENI Kabambe iliyofanywa na jeshi la Polisi Mkoani Tanga imefanikiwa kuwanasa watu 20 wasio waadilifu kwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo dawa za kulevya pamoja na wanaoendesha  biashara haramu za binadamu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini Jijini Tanga kuelekea s/kuu ya Eid Mubaraka.

Alisema kuwa katika operesheni zilizofanyika katika maeneo mbalimbali mkoani humo wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 20 kwa tuhuma kufanya vitendo vya uhalifu ambapo ni kosa kisheria.

Kamanda Mwaibambe alisema watuhumiwa hao wengine wamehusika tukio la kukamatwa na Bangi Kilogram 43, mirung kilo 75 pamoja na pombe haramu ya gongo lita 105 ambavyo vilikamatwa kwenye operesheni hiyo.

Alisema kwamba watuhumiwa hao walikamatwa baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema na kuzifanyia kazi na kufanikisha kuwanasa.

Aidha,alibainisha kueleza kuwa pamoja na hayo pia katika operesheni hiyo zimekamatwa pikipiki nane zilizokuwa zimeibwa maeneo mbalimbali mkoani Tanga.

Alisema kuwa taratibu zinaendelea mara baada ya upelelezi kukamilika watapandishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukuliwa dhidi yao.

Hata hivyo,Kamanda Mwaibambe alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka wananchi kuendeea kutoa ushirikia kwa jeshi la polisi ili kuweza kupunguza au kukomesha vitendo vya uhali mkoani hapo.
Mwisho.




 Pichani ni Ofisa kitengo cha Operesheni mkoani Tanga,ACP Zakaria Bernad  alipopata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari katika kikao hicho alieleza mpango kabambe umewekwa kufanya doria maeneo mbalimbali ikiwemo ya wananchi katika sherehe za Eid Mubaraka ili kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa jamii.

No comments:

Post a Comment