NA SOPHIA WAKATI,PANGANI
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Suleiman Mzee Suleiman amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Pangani kuwatumia Takukuru kuchunguza Miradi mitatu ukiwemo ukarabati wa Soko kuu Wilayani Pangani.
Suleiman alitoa maelekezo hayo juzi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza ambapo alisema kwamba, katika mradi huo wa soko amegundua taratibu za Serikali zimekiukwa juu ya suala la ushirikishwaji wa Wananchi kwenye Mradi huo.
Katika maelekezo yake, Suleiman aliyedai kuwa anatimiza jukumu hilo kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tanga,alisema,Takukuru wanapaswa kujua thamani na utafiti wa matumizi.

Alieleza kuwa baada ya uchunguzi wa Takukuru kukamilika taarifa yao iwasilishe ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani ndani ya Wiki mbili ili chama cha mapinduzi kuweza kujiridhisha.
Aidha,Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Tanga,Suleiman alisema, Pangani kuna changamoto nyingi ambapo uchunguzi wa kina unapaswa kufanyika akitaja ujenzi Jengo la ICU wilayani humo kuwa na utata licha ya kupata fedha kutoka serikalin mara mbili lakini halijakamilika.
"Takukuru tuanze uchunguzi wa kina Pangani yapo mengi. kuna suala hospitali ya wilaya zimeletwa fedha kutengeneza ICU fedha zimeisha na majengo kama yale yale yamejengwa maeneo mengine kwa fedha zile zile"alisema Suleiman.
Aliongeza kusema kuwa, katika ujenzi huo wa ICU Pangani shilingi 44 Milioni zimeongezwa pia jengo husika halijaisha huku akiwatakaTakukuru kuchunguza Mradi huo.
Mradi mwingine unaodaiwa kutafunwa wilayani Pangani aliutaja ni ule wa fedha kwa ajili ya matibabu kwa Wananchi juu ya ugonjwa wa Ngiri maji (Mabusha) ambapo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alitoa fedhi ili wananchi kutibiwa bure.
Awali Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah aliwataka Watumishi wa Serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea akiwasisitiza kubadilika na kufanya kazi kwa matokeo hatua aliyodai kuwa ndiyo itakayowabakiza kwenye nafasi zao.
Mkuu huyo wa wilaya pia aliwataka watumishi kuboresha suala la utoaji huduma kwa wananchi huku akisema Viongozi ni watumishi wa wananchi kazi yao ni kutatua kuwatumikia na kutatua kero zao.
Aidha, ametumia nafasi hiyo amemhakikishia Katibu huyo wa CCM wa Mkoa wa Tanga kwamba hatakuwa tayari kuona Ilani ya Chama cha mapinduzi CCM wilayani hapo ina tekelezwa.
"Siko tayari kuona Serikali ya CCM inadharauliwa kwa uzembe wa watu wachache.Naomba kuwepo na ushirikiano ili wilaya na nchi iweze kusonga mbele''alisema mkuu huyo wa wilaya ya Pangani Zainabu.
Naye Diwani wa Pangani Magharibi,Ramadhani Saburi alimweleza Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga kuwa,licha ya ujenzi wa Soko kuendelea lakini ushirikishwaji Kamati haupo hakuna Mwenyekiti wa Kijiji wala Mwananchi aliyeshirikishwa.
Kwa upande wake Diwani viti maalum Pangani mjini,Fatuma Issa alisema kwamba tangu kuanza kwa ujenzi wa soko hilo hawajashirikishwa lakini wamekuwa wakifuatilia na kutoa ushauri kwa mafundi ili kuhakikisha kukamilika kwa ujenzi wafanyabiashara na wanunuzi wananufaika.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani, Juma Hassan Mbwela aliahidi maagizo yote kuyafanyia kazi kwenye utekelezaji mradi huo wa Soko akisema madiwani watashirikishwa.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment