Thursday, 20 April 2023

MWENYEKITI WA CCM TANGA,RAJABU



Pichani mkono wa kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mloa wa Tanga,Rajabu Abdurahman akizungumza na mfanyabiashara wa nafaka soko la Ngamiani upatikanaji wa mazao na bei kwa wanunuzi,wa pili ni Meya wa halmashauri ya jiji la Tanga,Abdurahaman Shiloo.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tanga, Rajabu Abdurahman  amewataka Wafanyabiashara wa Vyakula kuepuka kutopandisha bei kwa dhana kuwa Ramadhan ndiyo mwezi wa kuweza kutajirika.

Hata hivyo,kimesema lengo ni kurahisisha kuondoa usumbufu kwa wananchi   na kuwataka kuendellea na msimamo wao wa kutopandisha bei kiholela kwenye kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Wito huo umetolewa juzi akiwa kwenye ziara ya siku moja kutembelea Masoko mawili la Ngamiani na Mgandini yaliopo katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Katika ziara hiyo, alipata fursa ya kuzungumza na wafanyabiashara kujua bei ya vyakula, bidhaa zinavyopatikana pamoja na kujua changamoto kwa wananchi.

Aidha Rajabu alisema, kwamba maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Viongozi wa Chama tawala na Chama CCM wanakuwa kimbilio la Wanyonge.

"Haya ni maelekezo ya Rais, Mwenyekiti wa CCM Taifa ametuhimiza kwamba tuhakikishe changamoto za wafanyabiashara na wananchi tuzitambue pia tuzitafutie majawabu zile ambazo ziko ndani ya uwezo wetu"alisema na kuongeza;

"Zilizo nje ya uwezo tuzipeleke sehemu husika ziweze kutafutiwa majawabu" alisema Abdallah huku akiwapongeza wafanyabiashara kwa kutopandisha bei vyakula.

"Kufanya biashara namna hii na mtapata thawabu, muendelee na msimamo huo na wananchi nao wasiwe na lawama nyingi kwa wafanyabiashara ambao nao hununua kwa wakulima waje wauze"alisema Abdallah.

Naye mfanyabiashara Shabani wa soko la Mgandini,Hussein Hoza alisema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ujazo kwenye ufungashaji bidhaa Shambani.

Pamoja na hayo alilalamikia kueleza kuwa uwepo wa vizuizi vya barabarani vinavyodaiwa kuwa vya halmashauri akivituhumu kukosa umakini katika utendaji.
Mwisho.


 

No comments:

Post a Comment