Pichani ni mgeni rasmi wa mashindano ya Tanga City Marathon 2017 mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kwea niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga,Martin Shigela akimkabidhi cheki ya sh.million moja Marico Serivesta kutoka JKT baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia muda wa dakika 57.00.23 kwenye mbio za kilometa 21,
NA SOPHIA WAKATI,TANGA.
Mashindano ya
Tanga City Marathon yaliyofanyika katika barabara mbalimbali za jiji la Tanga na kukomea viwanja vya Mkwakwani huku
Washindi wakikabidhiwa Zawadi za kitita cha pesa tasilimu za
kitanzania na medani.
Katika Mbio za umbali wa kilometa 21 kwa upande wa wanaume
Marico
Serivesta kutoka JKT amekabidhiwa kiasi cha shilingi Milioni Moja baada
ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia muda wa dakika 57.00.23,mshindi wa
pili Rameki Mombo kutoka Moshi amezawadiwa shilingi Laki 7 kwa kutumia dakika
57.00. 24, huku Mshindi wa Tatu Steven Guche kutoka Mburu mkoani Manyara amepata Laki 5 kwa kukimbia dakika 57. 7. 68.
Kwa upande wa Wanawake katika mbio hizo za kilometa 21
Nafasi
ya kwanza imechukuliwa
na Jakrini Juma kutoka JKT ambae amezawadiwa kitita cha Milioni Moja
baada
ya kutumia muda wa dakika 65.11.23,mshindi wa pili ni Sara Ramadhani
kutoka Arusha amezawadiwa Laki 7 kwa kutumia dakika 65.52.11 na mshindi
watatu
Anjerina Daniel kutoka Arusha amekabidhiwa shilingi Laki 5 kwa kutumia
dakika 66.26.53 kukimbia.
Kundi la tatu ni kilometa 10 kwa upande wa Wanaume
Mshindi
wa kwanza ni Emmanuel
Giniki kutoka JKT amepata shilingi Laki 7 kwa kutumia muda wa dakika
28.36.25, Akifuatiwa na Faraja Damas kutoka JKT amepata shilingi Laki 5
kwa kutumia dakika 28.57.83 huku mshindi wa tatu ni Augostino Sure ambae
amepata shilingi Laki 3 kwa kutumia dakika 29.18.39.
Kilometa 10 kwa upande wa Wanawake
Nafasi
ya kwanza imechukuliwa na Fraviana Matanga kutoka JKT ambae amepata shilibi Laki 7 kwa kutumia
muda wa dakika 33.6.89, Serina Isambu kutoka JKT amepata shilingi Laki 5 kwa kutumia
muda wa dakika 33.58.41 huku mshindi wa tatu Aisha Surum kutoka JKT amepata shilingi Laki 3 kwa kutumia muda wa dakika
34.57.7.
Hata hivyo kwa
Washindi walioshiliki kwa upande wa kilomita 10 mshiriki wa nne mpaka wa 10 wamepatia
shilingi 35,000 kila mmoja na Washiliki mbio za kilometi 21 wa nne mpaka wa 10
wamepatiwa kifuta jasho shiilingi 50,000 kila mmoja.na kwa upande wa
Viongozi walioshiriki wamekabidhiwa medani kwa kila Mmoja.
Mara
baada ya kugawa Zawadi kwa Washindi Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Thobias
Mwilapwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela
amewaomba Wadhamini hao kuendelea kudhamini Mashindano hayo ili kuleta
ushirikiano na mikoa mingine.
Hata hivyo mbio
hizo zenye makundi manne zimeshirikisha washiriki 500 kutoka mikoa
mbalimbali ikiwemo ya Arusha,Manyara,Singida, Zanzibar,Dar es alaam na
Tanga ambao ni wenyeji.
MWISHO..
Marico
Serivesta kutoka JKT mara baada ya kukabidhiwa cheki hiyo akionyesha kwa washiriki na mashabiki wa mchezo huo walioliojitokeza uwanja wa mkwakwani jijini Tanga.Pichani mkono wa kushoto mwanaume amevaa suti nyeupe ni mgeni rasmi,mkuu wa wilaya ya Tanga Mwilapwa akimkabizi cheki ya kitita cha million moja Jakrini Juma kutoka JKT baada ya kutumia muda wa dakika 65.11.23,akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo mdhamini mkuu wa mashindano hayo Sued Mkwabi na mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Tanga.
Pichani ni washiriki na baadhi ya mashabiki wa mchezo huo wakifuatilia zoezi la ugawaji zawadi kwa washindi na medani kwa washiriki wa mbio hizo.
Pichani ambaye amesimama amevaa fulana nyekundu ni mdhamini kuu wa mashindano ya Tanga City Marathon 2017,Sued Mkwabi akimvalisha medani mshiriki wa kundi la watu wenye ulemavu wa viungo.
Pichani mkono wa kushoto ambaye amevaa fulana nyeupe,ameshika kipaza sauti na karatasi ni mratibu wa mashindano hayo,Mwajasho awali akiwataja washindi na zawadi zilizopangwa kutolewa.
Pichani ni baadhi ya washiriki wa mbio za kilometa 21 wakiwasili viwanja vya mkwakwani jijini hapo.
Pichani ni baadhi ya washiriki ambao wamekimbia kilometa tano za kujifurahisha,katikati aliyevaa fulana ya njano ni muamuzi wa mpira wa miguu mkoani Tanga,Kudura Omari akiwa na washiriki wenzaki wakifuatilia mbio za kilometa 12.
Pichani ni mshindi wa kwanza mbio za kilometa 21 wanawake kabla ya cheki akikabiziwa medani.
Pichani katikati mwanamke ambaye amevaa fulana nyeupe ni mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Tanga,Elimina Murro akimpongeza baadhi ya washiriki wa mbio hizo,wakwanza mkono wa kulia ni mratibu wa mashindano hayo,Mwajasho akiwataja washiriki waliomaliza mbio hizo.
No comments:
Post a Comment