Pichani ni Mchungaji wa kanisa la Sabato Kana jijini Tang,Jackson Gladson akizungumza na waandishi wa habari (ambao hawako pichani)lengo la kuungana na madhehebu mengine kufanya kazi za kijamii eneo la Uhuru Park miaka 21 jijini Tanga.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KANISA la Sabato lililopo Kana Jijini Tanga limeshirikana na jeshi la Polisi kuimarisha Usafi wa mazingira huku Mchungaji wa kanisa hilo,Jackson Gladson akisema kufanya hivyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufili katika utendaji kazi wake huku mahusiano yakiimarishwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Mchungaji Gladson
alisema wameamua kutumia siku hiyo ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka
kuimarisha usafi wa mazingira kwa kushirikiana na jeshi la polisi
wakiamini kuwa ni njia mojawapo ya kuimarisha mahusiano sanjari na
kuboresha afya ya jamii.KANISA la Sabato lililopo Kana Jijini Tanga limeshirikana na jeshi la Polisi kuimarisha Usafi wa mazingira huku Mchungaji wa kanisa hilo,Jackson Gladson akisema kufanya hivyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufili katika utendaji kazi wake huku mahusiano yakiimarishwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Pichani ni kamanda wa polisi mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba mara baada ya kushiriki zoezi la usafi eneo la Uhuru Park miaka 21,jiji hapo akimpongeza mchungaji wa kanisa la Sabato Kana Jackson kwa hatua yake ya kuwaunganisha wakristo,madhehebu mengine ya dini na jeshi la polisi amesema mpango huo utasaidia kudumisha amani na utulivu miongoni mwa jamii ya wana Tanga.
Baadhi ya waumini wakifanya usafi.
Picha ni gari la kuondosha takataka lililotolewa na halmashauri ya jiji la Tanga liondosha uchafu.
Pichani ni miongoni mwa waumini wa madhehebu ya dini wakiendelea na zoezi la kugawa vitabu vya dini vyenye maelekezo ya mungu katika eneo hilo la Uhuru Park maarufu miaka 21 jijini Tanga.
Pichani ni waumini wa kanisa la Sabato Kana jijini Tanga wakisubiri kukusanya majani yanayofyekwa.
No comments:
Post a Comment