Pia, mchungaji wa kanisa hilo la Sabato kana jijini hapo,Jackson Mding’u alisisitiza kusema kuwa wanafunzi hao walitarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa Taifa hili ambapo aliwasihi watanzania kuendelea kuungana kudumisha upendo.
" Kanisa la sabato tutaendelea kumuunga mkono rais Dk.John Magufuli na kuonyesha uzalendo kwa wilaya na Taifa letu"
Pichani ni shehe wa Baraza la waislam (BAKWATA),Mohamed Mbaraka
akieleza kusikitishwa kwake na baadhi
ya mitandao ya kijamii kueleza katika ajali hiyo alinusurika Muislamu mmoja tu ambapo ameiomba serikali kuangalia namna ya kuwashughulikia
watu wa namna hiyo kwa sheria ya mitandao wanaoeneza lugha ambazo zinachangia
kupotosha jamii ya kitanzania akashughulikiwa kwa mujibu wa sheria iliyopo ili kulinda amani iliyojengeka.
Pichani ni mchungaji Msumari akieleza jinsi masikitiko yake kutokea kwa ajali hiyo.Pichani ni kaimu afisa elimu wa jiji la Tanga,Rose Ngowi akiwashauri walimu wa shule hiyo iliyokubwa na tatizo hilo,kipindi hiki kupeleka wainjiristi ili kuwatia moyo wanafunzi katika masomo yao.
Pichani ni mkuu wa wilaya ya Tanga,Tobias Mwilapwa akiungana na wanafunzi,walimu madhehebu ya dini kuomboleza.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KANISA la Wadventist Sabato Kana Central Jijini Tanga
limewaunganisha wanafunzi wa shule ya msingi Chuma,Indian Ocean na Kana Central
English Medium kufanya maombi kuhusiana na vifo vya vijana wenzao wa Jijini Arusha,pia wameishauri
Serikali kusimamia kwa makini vyombo vinavyotumika kusafirisha Wanafunzi.
Akisoma risala yao waliyoitoa kwenye maombi hayo jana iliyosomwa
na Braitiness Chaula wanafunzi hao walisema kwamba,wameshindwa kuvumilia kwa kukaa kimya
bila ya kusema lolote ambapo licha ya kupata fursa ya kufanya maombi pia
wameamua kutumia nafasi hiyo kuishauri serikali mambo kadhaa ya msingi.
Miongoni mambo walioishauri serikali yao,wanafunzi hao
walisema kuwa ingawa hawana weledi wa vyombo vya usafiri lakini wanadhani ni
vyema kwa serikali kuvifanyia uhakiki vyombo vya usafiri kuvibaini kama viko
salama kwa ajili ya kusafirisha abiria na wanafunzi hasa wale waliopo shule binafsi.
Aidha,wanafunzi hao walisema kwamba vyombo vya usafiri
ambavyo havijakaguliwa visiruhusiwe kufanya kazi huku wakitaka wanafunzi na magari
husika kukatiwa Bima kabla ya kuanza safari zao hatua ambayo itasaidia
kuimarisha usalama kwa watumiaji wa magari husika kwenye shule mbalimbali.
Mchungaji wa Kanisa la Sabato Kana jijini Tanga na mratibu,Jackson
Gladson Mding’u alisema lengo la kukutana kwa taasisi hizo za dini ni kuiunga
mkono Serikali katika kuomboleza vifo vya wanafunzi na watu wengine waliopoteza
maisha kwenye ajali hiyo iliyotokea Jijini Arusha na kuishtua jamii.
Alisema,ni muhimu kwa wanafunzi kufanya ziara wawapo shule
lakini kuna haja ya vyombo vya usafiri kuangaliwa ubora wake kabla ya kuanza
kazi huku madereva wanaowasafirisha wanafunzi hao wakiwa wale wenye ubora
unaokubalika jambo ambalo litasaidia kuondoa uwezekano wa ajali kujitokeza.
Aidha mchungaji huyo alisema kwamba
kumejengeka mazoea kwa baadhi ya matrafiki kutokagua magari ya wanafunzi na
badala yake kuyaacha jambo ambalo linaweza kusababisha ajali kujitokeza ambapo
amelishauri jeshsi la polisi kukagua kikamilifu magari ya abiria ili kuepuka
madhara.
Naye Shekhe Mohamed Mbaraka wa Baraza la waislam (BAKWATA)
ameelezea kusikitishwa kwake na baadhi
ya mitandao ya kijamii kueleeza kuwa katika ajali hiyo aliyenusurika ni
Muislamu mmoja tu ambapo ameiomba serikali kuangalia namna ya kuwashughulikia
watu wa namna hiyo kwa sheria ya mitandao.
Alisema mungu ni mmoja na hachagui ni vyema wanaoeneza lugha ambazo zinachangia
kupotosha jamii ya kitanzania akashughulikiwa kwa mujibu wa sheria iliyopo ili kulinda amani iliyojengeka.
Huku mchungaji wa kanisa la Sabato kana jijini hapo,Jackson Mding’u akisistiza kusema
kuwa ajali hiyo imegusa watu wengi ambao walitarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa
Taifa hili ambapo aliwasihi watanzania kuendelea kuungana kudumisha upendo.
Kwa
upande wake kaimu afisa elimu wa jiji la Tanga,Rose Ngowi amewataka
walimu wa shule hiyo iliyokubwa na tatizo hilo,kipindi hiki kupeleka
wainjiristi ili kuwatia moyo wanafunzi katika masomo yao.
Naye mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa
alisema,serikali itaendelea kuwa karibu na wananchi wake na itafuatiulia kwa makini ushauri uliotolewa
huku akitumia fursa hiyo kuliagiza jeshi la polisi kufanya ukaguzi kwa madereva
ambao wanajihusiaha na vitendo vinavyosababisha ajali kama ulevi.
Vilevile mkuu huyo wa wilaya ya Tanga alisema kwamba mkakati
madhubuti utawekwa kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wazembe
watakaopita kwenye alama za vivuko bila ya kuchukua tahadhari ya kusimama
akitanabaisha kuwa moja ya adhabu watakazopewa ni leseni kufungiwa.
Hata hivyo maombezi hayo yaliyofanyika shule ya
Kana Central English Medium kwa kuwaunganisha wanafunzi wa shule na madhehebu ya dini mbalimbali moani hapo.
Kana Central English Medium kwa kuwaunganisha wanafunzi wa shule na madhehebu ya dini mbalimbali moani hapo.
Mwisho.
Viongozi wakiomba.Wanafunzi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Tanga,juu ya madereva ambao watavunja sshria kwenye vivuko.,
Wanafunzi wakiimba mwimbo wa kuiombea Tanzania na rais Dk.John Magufuli.
Wanafunzi.
Pichani ni baadhi ya wanafunzi wakiwasikiliza viongozi wa dini mbalimbali.
No comments:
Post a Comment