Thursday, 18 May 2017

MAAFALI YA 20 KIDATO CHA SITA SHULE YA SEKONDARI MAZINDE JUU ILIKUWA HIVI,,

 Pichani katikati mwanamke ni Mkuu wa shule hiyo Sr. Evetha Kilamba,mkono wa kushoto ni mkuu wa wilaya ya Lushoto,January  Lugangika kulia ni kiongozi wa shule hiyo.

NA SOPHIA WAKATI,LUSHOTO
SHULE YA Sekondari ya St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo wilayani Lushoto, imewapongeza wazazi wanaosomesha watoto katika shule hiyo kwa kuweza kutoa michango iliyowezesha kupatikana maabara ya kisasa pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu.

Hata hivyo,uongozi wa shule hiyo unajivunia matokeo bora ya kidato cha sita tangu wameanza mwaka 1995 ambapo imekuwa ikifanya vizuri ikiwemo kutoa watoto bora katika masomo mbalimbali katika kumi bora Kitaifa.

Akizungumza juzi katika maafali ya 20 ya Kidato cha Sita, Mkuu wa shule hiyo Sister Evetha Kilamba, alisema kuwa ukarimu na michango iliyotolewa na wazazi imewezesha kupatikana nyumba hizo na maabara hiyo ya kisasa ambayo itawasadiai wanafunzi wanaohitimu kidato hicho mwaka huu, wakiwa wa kwanza kuitumia.

“Kiukweli mgeni rasmi napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru wazazi wanaosomesha watoto hapa Mazinde, kwa ukarimu wao na michango yao, kutokana na michango yao tumeweza kujenga nyumba za walimu na maabara ya kisasa,” alisema Sister Kilamba.

Pia,alieleza kwa kuainisha matokeo ya kidato cha sita tangu mwaka 2016, alisema mwaka huu walimaliza wanafunzi 136 ambao wote walikwenda Chuo Kikuu kutokana na madaraja waliyopata na shule hiyo ilishika nafasi ya 12 Kitaifa kati ya shule 423 na ya kwanza katika mkoa wa Tanga.

Sister Kilamba alisema pamoja na shule hiyo kufanya vizuri wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa vyumba vya walimu ambao kwa sasa wameongezeka baada ya uwingi wa wanafunzi ambao wameongezeka kutokana na ubora wa elimu inayotolewa.

Aidha alisema kwamba kuhitimu kwa Wanafunzi hao kunalifanya Taifa kupata ongezeko la wasichana 149 wanaomaliza kidato cha sita ambapo 109 wanahitimu kwa masomo ya Sayansi,uchumi 20 na Sanaa 20 ambapo alitanabaisha kwamba walimu wao wakiamini kuwa wote watafaulu vizuri.

Nae mkuu wa Wilaya ya Lushoto,January Lugangika ametoa siku sitini kwa taasisi binafsi  kuhakikisha zinafanya uhakiki wa  vyeti vya watumishi wao kama sehemu ya kuhakikisha watumishi hao wanatoa huduma bora na ya viwango kwa jamii.

Alisema kuwa zoezi la uhakiki wa vyeti bandia una faida kubwa hapa nchini na akawataka wanafunzi waliopo shuleni kuongeza bidii wakitambua maisha hayana njia ya mkato tofauti na kukaa darasani kusoma na kutunukiwa cheti halali kama ambavyo wanafunzi wa shule hiyo watakavyopatiwa.

Katika maafali hayo jumla ya wanafunzi 149 watahitimu masomo yao ambapo wanamaliza katika masomo ya sayansi ni 109, Uchumi 20 na wanamaliza kat8ika masomo ya sanaa ni 20.

Akizungumza katika maafali hiyo ambayo wazazi wengi hawakuhudhuria kama ilivyokusuidiwa kutokana na mvua kuharibu miundombinu ya barabara ya kwenda Lushoto.
Mwisho.

 Pichani ni viongozi mbalimbali wakifuatilia burudani siku ya maafali hayo ya kidato cha sita.




 Pichani ni miongoni mwa wahitimu wa kidato cha sita 2017 wakiwasikiliza viongozi mbalimbali siku ya maafali hayo.
Pichani ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliobaki wakionyesha maigizo na burudani mbalimbali siku ya maafali.

No comments:

Post a Comment