Pichani ni Mkuu wa Idara ya uhamiaji mkoani
Tanga,Crispin Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya tukio lililotokea juzi saa 3:30 asubuhi baada
ya taarifa kutoka kwa raia wema waliowafahamisha maafisa uhamiaji ambao
walikuwa wakiwajibika kwenye mpaka wa Horohoro ambapo waliwafuatilia wahamiaji
hao.
NA SOPHIA WAKATI,MKINGA
WAETHIOPIA 45 wamekamatwa wakiwa
wamejificha kwenye mashamba ya Wananchi huko kijiji cha Horohoro wilayani
Mkinga mkoani Tanga ambapo walikuwa wakimsubiri mtu aliyekuwa akiwatorosha
wakati wa kifanya safari yao ya kuelekea Afrika kusini walikodai kuwa wanakwenda
kutafuta maisha.
Mkuu wa Idara ya uhamiaji mkoani
Tanga,Crispin Ngonyani amesema kuwa tukio hilo limetokea saa 3:30 asubuhi baada
ya taarifa kutoka kwa raia wema waliowafahamisha maafisa uhamiaji ambao
walikuwa wakiwajibika kwenye mpaka wa Horohoro ambapo waliwafuatilia wahamiaji
hao.
Alisema,wahamiaji hao baada ya
kukamatwa walisema walikuwa kwenye mashamba hayo wakiwa wanamsubiri aliyekuwa
akiwasafirisha ambaye alikuwa akikagua njia ili kuweza kupita pasipo kutiwa
nguvuni ambapo taarifa zinaeleza kuwa kwenye maeneo hayo waliharibu mazao ya
wananchi.
Mkuu huyo wa Idara ya uhamiaji
alisema kwamba raia hao wa Ethiopia kwenye mashamba hayo walikutwa wakivuna
mahindi mabichi na kuyala mazingira ambayo huenda yakawa yamesababishwa na njaa
ambayo ilikuwa ikiwakumbua ndipo wananchi kuwafahamisha askari ambao
waliwakamata.
Aidha mkuu huyo wa uhamiaji
alisema,vitendo vya uhamiaji usiozingatia sheria limekuwa likiongezeka ambapo
jitihada zitaendelea kufanywa kuwapatia elimu wananchi ili kusaidiana na
serikali kupiga vita matukio ya aina hiyo ambayo kwa upande mwingine yanaweza
kuchangia kuhatarisha usalama.
Kwa mujibu wa afisa huyo,Ngonyani
alibainisha imekuwa ni kawaida kwa Waethiopia hao kudai wanapita kama njia
kwenda Afrika kusini kwa ajili ya kutafuta maisha ambapo ameishauri jamii
kuendelea kushirikiana kwa karibu na uhamiaji lengo likiwa kuondosha kabisa
vitendo hivyo visivyozingatia misingi ya sheria.
Hata hivyo,pamoja na kiongozi huyo
wa uhamiaji alisema kwamba wapo baadhi ya watu ambao wanajihusisha na kuishi
nchini kinyume na taratibu za sheria baada ya vibali vyao kuisha muda ambapo amewasihi
watu wa namna hiyo kufuata taratibu kabla hawajabainika na kuchukuliwa hatua za
kisheria ikiwemo ile ya kulipa faini na kufungwa jela.
Vilevile alisema kwamba katika
kuhakikisha kuwa wanadhibiti vitendo hivyo idara ya uhamiaji mkoani Tanga
imeweka Vizuizi barabarani maeneo ambayo upekuzi hufanyika lengo likiwa
kuwabaini wahamiaji hao wasiozingatia sheria huku akiwasihi wale ambao vibali
vyao vimeisha kufuata utaratibu stahiki.
Hata hivyo,pia alitumia nafasi hiyo
kwa kuwataka wananchi wanaoshi pembezoni mwa mpaka wa nchi jirani Kenya kuendelea
kuwaamini na kutoa ushirikiano lengo likiwa kudhibiti vitendo vya uhamiaji
mkoani hapo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment