Pichani ambaye amesimama ameshika kipaza sauti ni mbunge wa jimbo la Muheza,Adadi Rajabu juzi akielezea jinsi alivyofanikiwa kufanikisha ujenzi ea madarasa matatu ya shule ya msingi Kiwanda kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wilayani hapo baada ya kusikiliza kilio chake juu ya shule hiyo.
NA SOPHIA WAKATI,MUHEZA
MBUNGE wa Jimbo la Muheza CCM,Adadi Rajabu amefanikisha
ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa ya shule ya msingi Kiwanda kata ya Tongwe hatua
ambayo imesaidia kuboresha miundombinu hiyo ya elimu pamoja na kuwahakikishia usalama
wanafunzi waliokuwa wakisoma kwenye majengo mabovu.
Hayo yamebainika jana kwenye hafla fupi ya kukabidhiana
majengo hayo ambapo Mbunge huyo alieleza kwamba lifikia uamuzi wa kuijenga
shule hiyo baada ya kufanya ziara kwenye eneo hilo na kubaini kwamba ilikuwa
chakavu kwa majengo yake kuwa mabovu na hivyo kuhatarisha usalama wa watoto.
Ili kufanikisha ujenzi huo mbunge huyo alichangia kiasi cha
Tsh 9.4 milioni huku halmashauri na wananchi nao wakichangia ambapo hadi mradi
huo wa ujenzi kukamilika zilitumika Tsh 26,470,800/= huku wafadhili Muheza
Development Trust Fund ‘MDTF’ ukiwezesha kupatiakana kwa Tsh 9.8.
“Baada ya kukuta shule ni chakavu niliagiza ivunjwe haraka
ili kuimarisha usalama,nikawatafuta wadau Muheza Developmnt Trust Fund MDTF
kuomba ufadhili wa ujenzi huo wakatoa Tsh 9.18 milioni huku halmashauri wakitoa
Tsh 10.4 na wananchi nguvu kazi,naomba myatunze majengo haya”alisema.
Aidha mbunge huyo alisema kwamba kukamilika kwa mradi huo na
mingineyo wilayani Muheza ni matokeo ya ushirikiano wa karibu na wananchi
sambamba na wadau wengine huku akielezea kufanikiwa kujenga Visima vya maji
vipatavyo 25 na hivyo kupunguza changamoto ya upungufu wa maji.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo mwalimu mkuu wa shule
hiyo,Elia Chamungwana alisema shule ilijengwa 1924 na kanisa la Anglikana ambapo ilitumika
kama chuo cha ualimu na mwaka 1992 chuo kilihamishiwa Korogwe ambapo sasa
shuleni hapo kuna upungufu wa walimu 3 na matundu ya vyoo.
Vilevile alisema kuwa hali ya chakula shuleni sio nzuri
ambapo wazazi wanachangia kiasi cha kilo mbili za mchele kwa miezi mitatu
utaratibu ambao utaendelea huku akisistiza kusema kwamba hali hiyo itabadilika
katika kipindi hiki ambacho mavuno yataanza kupatikana baada ya msimu huu wa
mavuno.
Kwa upande wake mwenyekiti wa MDTF Farough Baghoza alisema
kwamba hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuunga mkono
jitihada za Rais kufikisha huduma za msingi kwa sehemu kubwa ya jamii akisema
amefarijika kuona watoto wa kitanzania wanapata eneo stahiki la kuweza kujifunzia.
Kwa mujibu wa Baghoza shirika la MDTF limeonyesha dhamira ya
dhati katika kuwahudumia ambapo lengo la Rais linaungwa kwa mkono ikiwemo sera
ya elimu bila malipo kwa watoto wa kitanzania ambapo aliwasihi wazazi
kushirikiana kwa karibu na walimu kuhakikisha watoto wanasoma vyema.
Mwisho.
Pichani katikati ni mkuu wa moa wa Tanga,Martin Shigella,kushoto ni mbunge wa jimbo la Muheza Adadi Rajabu,akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Peter Jmbele,na mkono wa kulia mwanamke ambaye amevaa baibui jeusi ameshika karatasi ni mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo akifuatiwa na katibu tawala mkoa wa Tanga,Zena Said wakifuatilia wasanii wakitoa burudani mbalimbali juzi katika hafla ya ufunguzi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Kiwanda wilayani Muheza.. Pichani ambaye amevaa kazu amesimama ameshika karatasi ni mwenyekiti wa MDTF,Farough Baghoza alipopewa nafasi akieleza kwamba hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuunga mkono jitihada za Rais kufikisha huduma za msingi kwa sehemu kubwa ya jamii akisema amefarijika kuona watoto wa kitanzania wanapata eneo stahiki la kuweza kujifunzia.
Mkuu wa mkoa akimkabidhi cheti mwenyekiti wa MDTF miongoni mwa wadau waliofanikisha ujenzi huo.
Pichani kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya Muheza,Luiza Mlelwa akiwasalimia viongozi mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa cheti kwa kufanikisha na ufuatiliaji wa ujenzi huo.
Pichani ni baadhi ya wananchi wa kijiji cha kiwanda wakiwasikiliza viongozi siku ya hafla ya ufunguzi wa madarasa hayo.
Pichani ambaye amesimama ni mkuu wa wilaya ya Muheza,Mwanasha Tumbo awali ofisini kwake akiwasilisha taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Tanga akiwa na viongozi mbalimbali.
Pichani ni mkuu wa mkoa wa Tanga,Akifungua madarasa hayo.
Pichani ni mkuu wa mkoa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na baadhi ya watoto 42 wa darasa la awali mara baada ya kulifungua.
No comments:
Post a Comment