Pichani ni kamanda wa polisi mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba akizungumza na waandishi wa habari hawako pichani kuelekea s/kuu ya Eid elfitri ,
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI
la polisi mkoaniTanga,limepiga marufuku watu wanaojiandaa kuendesha
disko toto katika kumbi mbalimbali za starehe wakati huu wa kuelekea
sikukuu ya Eid
elFitri mkoani hapo,huku likiwataka waache kufanya hivyo vinginevyo
watachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ofisini kwake,Kamanda wa polisi mkoa wa
Tanga,Benedict Wakulyamba, alisema kuwa jeshi lake limejipanga kuweka
ulinzi katika maeneo ya kumbi za starehe,
nyumba za ibada pamoja na fukwe za bahari wakati huu wa sikukuu.
“ Tumetoamaelekezokwawananchiwet uwotemkoaniTanga,
kwambatumepigamarufukukuendesh adisko Toto katikamaeneoyoteyamkoa, anayefanyamaandaliziaachemaram oja, mambo hayonikinyume cha maadili yetu lakini pia ni kinyume cha sheria,”alisemaKamandahuyo.
Pia
kamanda huyo wa polisi alisema kuwa ni marufuku kwa watoto kukutwa
wakiogelea bila ya kuwa na wazazi
au walezi watakaowaangalia katika sikukuu na kwamba kufanya hivyo
wakikutwa wazazi ndiyo watawajibika kwa kushitaki kwa vyombo vya
kisheria.
Kamanda
huyo alisema pamoja na watoto kukatazwa kuogelea lakini pia watu wazima
wametakiwa waache mara moja kwenda kuogelea katika maeneo ambayo
hayajatengwa rasmi kwa watu kuogelea na badala yake wakaogelee katika
maeneo maalum yanayojulikana.
Hata hivyo,Kamanda huyo pia alihadharisha wazazi wawe makini katika kutunza na kuwalea watoto wao katika kipindi hiki
cha sikukuu na kwambae ndapo kutaokotwa mtoto amepotea,mzazi atawajibika kisheria na kupotea kwake mtoto huyo.
“Kiukweli tunatoa angalizo kwa wazazi wawe makini na watoto katika sherehe hizi za Eid
elFitri,mtoto akipotea mzazi atawajibika yeye mwenyewe sababu jukumu la
kuleana kutunza mtoto ni la mzazi, sasakwaniniumuachehadiapotee,”
alisema Kamandahuyo.
Katika
hatua nyingine jeshi hilo limetoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto
kuahakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani katika kipindi
hiki
cha sikukuu ikiwemo kujiepusha na unywaji wa pombe huku wakiendesha
vyombo hivyo kwa kuata sheria iliyopo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment