Pichani ni kamanda wa polisi mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba akiwaeleza waandishi wa habari (hawako pichani) jinsi walivyofanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya wafanyabiashara wawili walikutwa wamekufa nyumba ya kulala wageni Bomai Inn jijini Tanga.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la Polisi Mkoani Tanga.linamshikilia mfanyabiashara, Ismail Yahaya
Muhaji (41) mkazi wa Bulwa Amani wilayani Muheza,Dar e salaam na Tunduma mkoani
Songwe akituhumiwa kuhusika kwa Mauaji ya watu wawili.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakuyamba amethibitisha kukamatwa
kwa mtuhumiwa huyo akisema, kuwa mtuhumiwa tayari yuko mikononi mwa Polisi kwa
mahojiano ili kujua kiini cha mauaji hayo.
Alisema, mtuhumiwa ambaye ana makazi yake huko Bulwa Amani Muheza, Dar es
Salaam na Tunduma Mkoani Songwe anahusishwa na mauaji ya Septemba 25 mwaka huu
wa 2017 jijini hapo.
Kamanda,Wakulymba alisema kwamba katika kipindi hicho kulitokea mauaji ya
kutatanisha kwenye nyumba ya kulala wageni ya Bomai Inn iliyopo Jijini Tanga.
Kutokana na tukio hilo jeshi la Polisi liliendelea na uchunguzi hadi
kufanikiwa kumnasa mtuhumiwa huyo mkoani Mwanza ambaye anaendelea kushikiliwa kwa uchunguzi.
Aidha Kamanda Wakulyamba alitanabaisha kwamba katika mahojiano mtuhumiwa amekiri kutenda
tukio hilo la kusikitisha kwa Jamaa zake hao waliofariki dunia.
Alisema mtuhumiwa (Muhaji) amekiri kuwapa kilevi kikali (Valium)
marehemu hao wawili kwa kutumiwa mwanya wa ukaribu nao katika biashara
walizofanya.
Hata hivyo alisema, mtuhumiwa huyo tayari ameshafikishwa Mahakamani huku
upelelezi ikiendelea kujua kisa na chanzo cha mauaji hayo ya kikatili.
Kamanda huyo wa jeshi la Polisi Mkoani Tanga alisema jeshi la Polisi
litaendelea kuwakamata wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili
haki kuweza kutendeka na amani kuimarika.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment