Wednesday, 21 October 2026

COPRA YANG’ARA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA UBUNIFU WA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO

“Tumepata tuzo ya ushindi kwa ubunifu tulioufanya. Tunastahili tuzo hii kwa sababu tumezingatia kaulimbiu ya mwaka huu inayosema Ubunifu wa leo, lishe bora ya kesho kuelekea Dira 2050,” alisema Sapanjo
NA SOPHIA WAKATI, TANGA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imeibuka na ushindi katika maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani baadae ya kupika Mtori wa kutuma  Choroko. ,Yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Usagara,mkoani Tanga, baada ya kufanya shughuli mbalimbali za kibunifu zinazolenga kuongeza thamani ya mazao na kuboresha lishe.

Ushindi huo umetokana na ubunifu uliofanywa na COPRA, ikiwemo kuonesha mapishi ya vyakula vinavyotokana na jamii ya mikunde pamoja na kuwashirikisha wadau wanaojihusisha na kuongeza thamani ya mazao kuonesha bidhaa na kazi zao.

Alisema kupitia banda lao, walifanya shughuli mbalimbali za kibunifu, ikiwemo kuonesha mapishi ya vyakula vya jamii ya mikunde na kuwapa nafasi wadau wa kuongeza thamani ya mazao kuonesha kazi zao.

Sapanyu alieleza kuwa COPRA pia ilitumia maadhimisho hayo kuwakutanisha wadau wa minyororo ya thamani ya mazao ya viungo ili kusikiliza changamoto zinazowakabili na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta hiyo.

Alisema baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na wadau zinahusu uzalishaji, uhifadhi na masoko ya mazao, ambazo zinahitaji kushughulikiwa ili kuwawezesha wakulima na wadau wengine kunufaika zaidi na shughuli zao.

Aliongeza kuwa COPRA inalenga kuimarisha minyororo ya thamani ya mazao yote inayoyasimamia, yakiwemo mazao ya viungo, kwa kuhakikisha yanazalishwa kwa ubora na kuwa na masoko.

"COPRA imejinga kuimarisja sekta ya kilimo,kuongeza thamani ya mazao,kusaka masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi,kuondoa changamoto kukosa wanunuzi"alisema Martin.

Maadhimisho hayo yalifungwa Oktoba 16, 2026, na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Salha Burian, aliyemwakilisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dk. Bashiru Ally Kakurwa.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment