Wednesday, 21 October 2026

WANANCHI WA PANGARAWE KATA YA GOMBERO WAMUOMBA MBUNGE WAO KUIWASAIDIA KUTATUA KERO YA ARDHI.


Picha ni miongoni mwa wananchi wa Pangarawe kata ya Gombero wilayani Mkinga wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.

NA SOPHIA WAKATI,MKINGA

MBUNGE wa Jimbo la Mkinga,Twaha Mwakioja amekusudia kuanza ziara kijiji kwa kijiji kusikiliza kero za wananchi hususani migogoro ya ardhi ili kuweza kuziwasilisha ngazi husika na kuzipatia ufumbuzi.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya wananchi wa kitongoji cha iPangarawe,Rubawa kijiji cha Gombero kuniandikia barua Mbunge wao wakilalamikia kukopwa mwa maeneo ya ardhi.

Kupitia barua hiyo,kwa Mbunge ambayo ambayo Uhuru nakala yake inayo wamezibainisha kero zinazowakabili kuwa ni kutoitishwa ya mapato na matumizi.

Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na mwandishi wa hii ,Mbunge Mwakioja alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya kuzifahamu kero hizo alikiri kusikia miongoni.

Alidai kuwa amesikia miongoni na kwamba hajapata taarifa rasmi huku akiahidi kufanya kufanya mikutano ya kijiji kwa kijiji kusikiliza kero ili kupata ufumbuzi.

Akitoa ufafanuzi juu  wananchi wa kijiji Cha Gombero kitongoji cha Pangarawe kata ya Gombero wilayani Mkinga wakilalamikia ukosefu wa mikutano ya taarifa za mapato na matumizi, wakimtaka Mbunge wao kuingilia kati ili kupata utatuzi juu ya kero zinazowakabili ikiwemo migogoro ya ardhi.

Katika taarifa yao kwa waandishi wananchi hao walisema,Yusufu Hamisi na Iddi Ally walisema kwa kipindi kirefu sasa tangu 2025 licha ya kukabiliwa na kero mbalimbali lakini zimekosa kupata ufumbuzi.

Nae Kassim Hassani na Hadija Simba wakazi wa Pangarawe walisema, Rais Dk.Samia Suluhu Hassani anazamira nzuri kuleta mradi wa chuo cha Mzumbe Mkinga kuleta fursa kwa wananchi.

Walisema kuna suala la changamoto ya kutokufahamika kwa miradi iliyopo kwenye kijiji hicho,mipaka inashindwa kufahamika ilipoishia na hata kupitishwa na Wadau kijijini.

Kero nyingine ni Wananchi kutokufamishwa namna ambavyo watanufaika na mradi ujenzi chuo Kikuu cha Mzumbe licha ya kuwa wametoa eneo lao kwa ujenzi wa mradi huo.

Aidha kuna kero ya uuzwaji holela wa maeneo ya ardhi wakiwatuhumu baadhi ya viongozi wa Kijiji kushirikiana na madalali kuuza maeneo ya Wananchi hao ndani ya kitongoji cha Pangarawe.

Changamoto nyingine ni juu ya Wakazi wa Pangarawe,Rubawa na Mwamkongo kudai kupatiwa hadhi ya kijiji tangu mwaka 2025 na sintofahamu ya mipaka kati ya Tanga na Mkinga kwa lengo la Gombero ambapo wamedai kuwa mpaka huo umekuwa ukihama.
Mwisho. 







Miongoni mwa Wananchi wa Pangarawe kata ya kigombe wilayani Mkinga Mkoani Tanga wakilalamikia kero mbalimbali ikiwemo ya Ardhi



No comments:

Post a Comment