Friday, 6 November 2026

PANGANI WAKAZI WA KIJIJI CHA KIGURUSIMBA KUPISHA ENEO LA SHAMBA LA MIVUMONI KWA HIARI KUPISHA UHAKIKI WA ENEO

Picha ni Mkuu wa mkoa wa Tanga,Dk.Batlida Salha Burian akiwahutubia wananchi wa Kijiji Cha  Kigurusimba wilayani Pangani.

 

NA SOPHIA WAKATI, PANGANI

WAKAZI wa Kijiji cha Kigurusimba waliokuwa wamevamia eneo la Shamba la Mivumoni, wametakiwa kuondoka na kusitisha shughuli kwa hiari ili kuapisha uhakiki wa mipaka katika shamba Hilo.   


Huku Mwenyekiti wa Kijiji, Syvestre Munga, akisema wavamizi hao, walipewa na uongozi wa kijiji kwa nyakati tofauti zilizopita wakiamini ilikuwa nje ya eneo la Shamba.


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dk. Batilda Salha Burian, kwenye mkutano wa hahdara alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kigurusimba wilayani Pangani.


Poa ameiagiza halmashauri ya Wilaya ya Pangani, kufuta hati miliki za kimila za Pangani Plantation Ltd, Mamba Ranchi Ltd na watu binafsi, waliopewa ardhi kinyume cha Sheria, wakihalalisha umiliki wa eneo kwenye Shamba la Mivumoni.


Mkuu huyo wa Mkoa wa Tanga pia ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa  TAKUKURU. kufanyia uchunguza mchakato uliowezesha kutolewa kwa ardhi na hatimiliki hizo.

 

Balozi Dk. Batilda, alifanya ziara katika eneo hilo lenye mgogoro na maagizo hayo,ni katika mkutano wa hadhara na wananchi wakiwemo wale waliovamia eneo hilo huku wakiendesha shughuli mbalimbali za kibinadamu.


Balozi Dk. Batilda alisema, baada ya Wizara ya Kilimo kupitia uongozi wa Shamba la Mivumoni (VVBD/TVLA) kuafiki kuachia hekta 1,271 zilizovamiwa, watu wanaoishi ndani ya eneo lililobaki lenye ukubwa wa hekta 4,079 wanapaswa kuondoka kupitia utaratibu maalum utakaoanza kutekelezwa Novemba 7, 2026.


Akizungumza baada ya kupata fursa Meneja wa VVBD/TVLA Dk.Oliva Manangwa, amesema, uongozi wake uko tayari kutoa ushirikiano utakaofanikisha kuwahamisha watu waliovamia kwenda kwenye eneo bora litakalopangwa kwa ajili yao.


Amesema kwamba,eneo hilo ni lile lenye ukubwa wa hekta 1,271 ambalo halitawahusu wanaoishi humo pekee, isipokuwa na wale ambao makazi na shughuli zao zimo ndani ya eneo lililosalia.


Amesema kuwa, ikitokea kuna mkazi ama wakazi wenye eneo au maeneo yanayozidi ukubwa utakaobainishwa na wataalamu wa upimaji wa ardhi kwa kila kaya, watalazimika kupunguziwa ili kukidhi mahitaji ya wengine.


Kwa mujibu wa Dk.Manangwa, shamba hilo lina maslahi mapana kwa Taifa likitumika kufanyia majaribio ya chanjo za mifugo zinazotengenezwa na Kituo cha Chanjo (TVI) Kibaha mkoani Pwani.


Aidha amesema kuwa eneo hilo linatumika kufanyia majaribio ya viuatilifu kwa ajili ya usajili, shamba darasa kwa wadau wakiwemo wafugaji na wanafunzi wa fani ya mifugo sanjari na kutumika kwa tafiti zinazoihusu sekta hiyo.

Mwisho

                    










No comments:

Post a Comment