Thursday, 29 August 2024

HALMASHAURI ZA MKOA WA TANGA ZATAMBA KUYATUMIA MAONYESHO YA NANE NANE 2024 KUTANGAZA FURSA ZILIZOPO

 

Pichani ni Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mkinga Faizu Nyoni akionyesha miongoni mwa mazao yanayolimwa wilayani humo

NA SOPHIA WAKATI,MOROGORO

WAJASIRIAMALI kutoka wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, wameyatumia maonesho ya Kilimo nane nane kwa mwaka huu katika kutanua wigo wa masoko hatua ambayo lengo lake ni kuongeza tija kwa uzalishaji wa bidhaa. 

 

Afisa Kilimo Mkinga,Faizu Nyoni ameyasema hayo  juzi Mkoani Morogoro kwamba, maonesho ya mwaka huu yameongeza elimu kwa wajasiriamali na pia kuwawezesha kutanua wigo wa masoko.

 

Alisema, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga  imewawezesha wananchi kada mbalimbali kushiriki maonesho hayo ili kuweza kujifunza vitu vingi huku wakibadilishana mbinu za uzalishamali.

 

"Tumekuja na wakulima ambao wamediriki kuchukua mbegu za mazao wakatumie kule tulikotoka, pia tumekuja na wajasiriamali mbalimbali wakiwemo vijana waliokopeshwa mikopo ya asilimia kumi" alisema.

 

Kwa upande wa vijana hao waliofanikiwa kupata mikopo ya asilimia kumi, afisa Kilimo huyo alisema, hao walinunua mashine kutengeneza masweta na kwamba  kuwepo kwao Morogoro kumewasaidia kuongeza wigo wa soko.

 

"Hapa wasiliamali tumewapa muda wanatembea kupata Connection wateja kuwa wengi" alisema afisa Kilimo huyo huku akitanabaisha kwamba Kilindi wanazalisha mazao ya biashara na chakula.

 

Amesema kwamba tayari wamefanya uhamasishaji wa zao la Korosho ambapo kwa kipindi cha mwaka jana wameanza matarajio yao yakiwa ni kutaka kuanzisha Amcos kwa sababu Korosho haziuzwi kwa njia za kawaida.

 

Pia wilaya ya Mkinga imeanzisha Kilimo cha zao la Pamba na pia wamekuwa wakizalisha lishe jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limesaidia kuiimarisha lishe ya wananchi hususani watoto.

 

Miongoni mwa wajasiliamali Duga Sigaya wilayani Mkinga,Elina Mumba amesema amenufaika na maonyesho ya nanenane kwa kutangaza bidhaa zake zinazotokana na zao la Muhogo na Korosho baada ya kupatiwa mikopo na halmashauri.

Mwisho


NA SOPHIA WAKATI,MOROGORO

WAKULIMA wa zao la Mkonge wilayani Mkinga wameiomba Serikali kuwaangalia wakulima wadogo kwa jicho la huruma katika kuwapatia mikopo ya muda mrefu, hatua ambayo itawawezesha kuendesha kilimo hicho kwa ufanisi. 

 

Meneja wa Kampuni ya Duvii Farm inayohusika na Kilimo na uchakataji Mkonge wilayani Mkinga, Robert Rashid Duvii alitoa Rai hiyo juzi kwenye kilele cha maonesho ya wakulima nanenane Mkoani Morogoro.

 

Duvii alisema kwamba maonesho hayo yamewasaidia wakulima mbalimbali kujifunza mambo mengi sambamba na kuona jitihada za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanaelimika.

 

Alisema kuwa, katika uzalishaji wa zao la.Mkonge manufaa makubwa yameanza kupatikana ingawa wakulima wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu sanjari na suala la mikopo kwa wakulima wadogo wadogo. 

 

Alisema, kwa mkulima mdogo ili kuweza kuangalia Shamba lake na kupata mazao yenye ubora inamchukua muda mrefu na mara nyingi wamekuwa wakikwama kwa kukosa mikopo ya muda mrefu.

 

"Kwa upande wa Mkonge Serikali iangalie namna ya kutoa mikopo ya muda mrefu,mkulima akishindwa kuangalia shamba vizuri atashindwa kupata product nzuri "alisema Duvii.

 

Akizungumzia changamoto ya miundombinu, Meneja huyo wa Duvii Farm alisema,pamoja na zao la Mkonge kwa sasa kuonekana kuwa na manufaa makubwa.Ukosefu mashine za uchakataji ni changamoto kwa wakulima.

 

Aidha Meneja huyo alisema, Duvii Farm wanazo mashine mbili ikiwemo ile ya kuhamahama 'mobile' huku wakiwa katika mchakato wa kununua mashine kubwa ya Korona itakayokuwa mkombozi kwa wakulima wadogo. 

 

"Sisi tunazo mashine mbili moja ni Moverable na nyingine ni Stored pale pale. Viwanda vikubwa vipo vichache na wakulima ni wengi nadhani bodi ya Mkonge walishaelezwa watafute mashine zao ili kusaidia wakulima" alisema Robert Duvii.

 

Pamoja na kuyasema hayo, Duvii alitumia nafasi hiyo kusema kuwa wanakusudia kuleta mashine kubwa itakayokuwa na uwezo wa kuchakata tani nne kwa muda wa saa moja na kwamba itakapokuja itakuwa mkombozi wa wakulima wa Mkinga.

Mwisho.



NA SOPHIA WAKATI,MOROGORO


WAKULIMA wa Matunda Wilayani Muheza Mkoani Tanga,wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwapatia mashine ya kuchakata machungwa hatua ambayo itawaepusha na changamoto ya mazao yao kuoza shambani.

Wametoa Wito huo jana wakiwa wanahudhuria maonesho ya Kilimo nanenane yanayofanyika Mkoani Morogoro, ambapo Richard Ismail wa Kata ya Songa wilayani Muheza mkoani Tanga,ameomba kuangaliwa uwezekano wa kujengewa kiwanda kidogo ili kuondoa changamoto hiyo kwa wakulima.

Ismail alisema kwamba, katika wilaya yao wamekuwa wakizalisha kwa wingi machungwa ya aina mbili huku akitaja Msasa na Valencia ingawa hapo awali pia walizalisha aina ya Jafa. 

Alisema kuwa, katika Kilimo hicho licha ya wananchi wengi kuhamasika lakini bado wamekosa kunufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na matunda wanayolima kuozea Shambani. 

"Tumefanikiwa kuzalisha kwa wingi Machungwa ila kwa ukdsefu wa mashine ama kiwanda kidogo,mengi huozea mashambani na hivyo tunapata hasara" alisema Mkulima huyo.

Pamoja na hayo ameishauri Serikali kupitia Halmashauri yao kuwatumia maafisa ugani katika kuwapatia elimu kabla mkulima hajapata hasara ya kwa wadudu kushambulia mazao yao na hivyo kuwaepusha na uwezekano wa kupata hasara.


Hata hivyo,Mkulima Ismail alielezea kuridhishwa kwake na hatua za haraka zinazoendelea kuchukuliwa na maafisa ugani katika kuwafikishia dawa wakulima wa zao la matunda.

Mbali na kuzungumzia biashara ya machungwa, Ismail alisema kuwa pia wamekuwa na utaratibu wa kuandaa miche na kuiuza kwa watu wanaohitaji  akisema katika kipindi cha mwaka 2022/23 waliandaa miche mingi huku akiwashukuru maafisa ugani kwa kuwapelekea madawa.

Kwa upande wa masoko kwa ajili ya kuuzia mazao yao,Ismail aliitaja mikoa ya  Dar es salaam, Mbeya, Pwani na nchi jirani ya Kenya ingawa alilalamikia changamoto ya madalali wanaoteremsha bei jambo ambali linaleta shida kwa mkulima na kukosa kipato stahiki.

Mwisho.

Mjasiriamali  Kata ya Mkata wilaya ya Handeni alivyoyatumia maonyesho hayo kutangaza bidhaa zake


NA SOPHIA WAKATI,MOROGORO

HALMASHAURI ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga imejidhatiti katika kutengeneza mazingira bora kwa Wafugaji wake hatua ambayo lengo lake ni kuwawezesha kupata mazao yenye ubora na hivyo tija kuweza kuongezeka.

Katika mikakati yao hiyo maeneo kadhaa yametengwa kwa ajili ya wafugaji zikiwemo hekta 22 zinazotumika kwa ajili ya kupata majani yanayotumika kama chakula cha mifugo hususani ng'ombe.

Mkuu wa idara ya kilimo  Ufugaji na Uvuvi Handeni Vijijini,Ibalila Chiza  anasema kuwa katika kuboresha sekta ya mifugo wanatekeleza zoezi la kuboresha Vinasaba kwa ng'ombe ambapo wanachagua ng'ombe bora wa kienyeji na kuwapandikiza na wale wa kisasa ili kupata matokeo bora.

Katika utaratibu huo, Chiza alisema wamefanikiwa kupata mbegu ya ndama wa miezi mitano akiwa na uzito 110 Kg hatua ambayo pia imesaidia kuongeza idadi ya wafugaji.

Hatua za namna hiyo zimeanza kuchukuliwa kwenye eneo la Msomera ambapi Halmashauri inaongeza nguvu ya ukusanyaji fedha kupitia mapato ya ndani kuboresha mifumo ya wafugaji

"Tumetenga maeneo na ranchi zipo kama tatu Handeni tunawakaribisha wawekezaji wa ndani waje kuwekeza kwenye mifugo"alisema Mkuu huyo wa idara ya Kilimo,Chiza. 

Ametaja faida zinazopatikqna kwa kutumia ng'ombe wa kisasa kuwa ni uzalishaji nyama na maziwa kwa wingi huku akitanabaisha kuwa upandikizaji ng'ombe kienyeji gharama zake ni zile za wastani.

Afisa huyo amemtolea mfano mmoja wa wakulima anayeitwa Shauri huko Kata ya Misima kwamba amepandikiza Ng'ombe 20 na 18 wamezaliwa na kwamba Mwaka mpya unaoanza zoezi litaendelea huku matarajio yakiwa kuwapoteza kabisa ng'ombe wasiokuwa na ubora.

Akizungumzia zao jingine la biashara wilayani Handeni kuwa ni Mkonge ingawa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa.mashine ya.kuchakata zao hilo na kupata bidhaa ya nyuzi bora zinazohitajika sokoni.

Pia alisema, wamekuwa wakijishughulisha na kilimo cha zao la matunda ambayo huingizia fedha nyingi Halmashauri ambapo wangetamani kuwa na kiwanda cha kuongeza thamani matunda.

Pamoja na hayo kuna zao mama la mahindi asilia linqlotukika kwa chakula na biashara ambapo kuna mwekezaji mmoja mwenye kiwanda cha nafaka bado anahitaji mwekezaji eneo hilo.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment